TANESCO yapewa saa 24 tatizo la umeme Kigoma

0
181

Waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani ametoa saa 24 kwa TANESCO mkoani Kigoma kukamilisha matengenezo ya mashine mbili zilizoharibika ili kumaliza tatizo la umme katika manispaa ya Kigoma Ujiji.

Akizungumza mara baada ya kukagua mashine hizo Dkt. Kalemani amesema tatizo la kukatika kwa umeme katika manispaa hiyo halitokani na ongezeko la matumizi kama ilivyoelezwa awali na TANESCO bali ni ubovu wa mashine mbili kati ya tano zinazotegemewa kuzalisha umeme kwenye eneo hilo.

“Nataka kupata maelezo ni kwanini injinia anasema mashine zote zinafanya kazi wakati mashine mbili ni mbovu wewe kaimu MD baki hapa siku tatu hadi umeme utengamae,” amesema Kalemani.

Aidha ameitaka TANESCO kuhamisha mashine nyingine mbili katika vituo vya Ngara mkoani Kagera na Loliondo mkoani Arusha kuzifunga Kigoma ili kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawati 8 hadi megawati 10 na kuufanya mkoa huo kuwa na ziada ya megawati mbili za umeme.