Jezi za Simba zaanza kuuzwa

0
2194

Klabu ya Soka ya Simba imetangaza kuanza kuuza jezi mpya leo Septemba 3, 2021 zitakazotumiwa na klabu hiyo kwa msimu wa mwaka 2021/2022.

Kuanza kuuzwa kwa Jezi hizo kunakuja siku moja kabla ya uzinduzi rasmi wa jezi hizo kutokana na mahitaji ya mashabiki wa klabu hiyo.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga amewaambia waandishi wa habari kuwa jezi hizo zinapatikana nchi nzima.

Aidha, Kamwaga amesema kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayosindikiza Wiki ya Simba ambayo inatarajiwa kuadhimishwa kuanzia Septemba 13 mpaka Septemba 19 kwenye hafla ya kilele cha siku ya Simba.

Kuhusu kuvuja kwa Jezi ya Klabu hiyo, Kamwaga amesema sio jambo la ajabu na hata vilabu vikubwa barani Ulaya vimekuwa vikikabiliwa na tatizo hilo.