Mwakinyo atamba kutetea mkanda wake

0
2003

Bingwa wa Umoja wa Ngumi Barani Afrika (ABU) Mtanzania Hassan Mwakinyo ametamba kutetea mkanda wake kwa kumchakaza mpinzani wake bondia Julius Indongo kutoka Namibia, katika pambano la mizunguko 12 litakalofanyika hapo kesho mkoani Dar es Salaam.

Mwakinyo ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa zoezi la kupima uzito na kuongeza kuwa, hali yake ya kiafya na maandalizi yake yanatosha kumshinda mpinzani wake.

Kwa upande wake Julius Indongo amesema kuwa amejiandaa vema kunyakua mkanda huo, licha ya maandalizi hayo kufanyika katika kipindi ambacho kumekuwa na maambukizi makubwa ya corona nchini Namibia.

Kwa upande wake Promota wa pambano hilo Amos Amoma amesema, mapambano hayo yanalenga kupeleka mchezo wa ngumi katika anga za kimataifa, na amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia mpambano huo.

Kabla ya Hassan Mwakinyo na Indongo kupanda ulingoni kutakuwa na mapambano kadhaa ya utangulizi, likiwemo lile la Tony Rashid kutoka Tanzania ambaye atapanda ulingoni kumenyana na Bongane Mahlangu kutoka Afrika Kusini kuwania mkanda wa ABU.