Kesi ya Mwakabibi yatajwa tena

0
167

Aliyekuwa Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam Lusabilo Mwakakabibi na mwenzake Edward Haule ambaye alikuwa mratibu wa mradi wa DMDP, wamefika katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu ambapo kesi yao imetajwa kwa mara ya pili.

Katika kesi ya msingi ya uhujumu uchumi namba 63 ya mwaka 2021, Mwakabibi na mwenzake wanakabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la matumizi mabaya ya ofisi na matumizi mabaya ya madaraka.

Hakimu anayesikiliza shauri hilo ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 30 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa, baada ya Wakili wa Serikali kudai upelelezi wake bado haujakamilika.

Hata hivyo Upande wa utetezi unaowakilishwa na Wakili Jeremiah Mtobesya umeomba upande mashtaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo, ili washtakiwa waweze kupata haki zao za msingi.