TANESCO yaboresha huduma Nanyumbu

Miundombinu

0
267

Katika kuimarisha utoaji wa huduma wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani humo, limejenga jengo la kutolea huduma mbalimbali za umeme kwa Wananchi.

Jengo hilo ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 90 na kutumia shilingi milioni 189 hadi sasa, linakadiriwa kugharimu shilingi milioni 307.2 hadi kukamilika kwake.

Hayo yameelezwa na msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo Laura Hyera, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi uliofantwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Luteni Josephine
Mwambashi.

Hyera amesema mradi huo ulianza kutekelezwa mwezi Septemba mwaka 2020, na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Amesema mradi huo ambao umeanza kunufaisha Wananchi wa Nanyumbu kwa kutoa ajira kwa mama lishe , mafundi wa ujenzi pamoja na walinzi.

Akiongea mara baada ya kuweka jiwe la Msingi, Luteni Mwambashi amesema ujenzi wa mradi huo unaenda vizuri, huku akiwataka wasimamizi kusimamia kikamilifu fedha na hatua nyingine ili kuhakikisha jengo linakamilika na kuanza kutoa huduma kwa Wananchi.