NIC yaipiga jeki shule ya Sekondari Jitegemee

0
155

Shirika la Bima la taifa-NIC limetoa Msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kukarabati Mabweni ya Shule ya Sekondari Jitegemee iliyoko Mkoani Dar es salaam.

Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 26 utatumika katika ukarabati wa mabweni ya wavulana katika shule hiyo kwa lengo la kuwaondolea adha ya ubovu wa mabweni hayo.

Mkurugenzi wa Masoko wa NIC Yesaya Mwakifulefule amsema msaada huo ni sehemu ya mchango wa shirika la Bima katika kusaidia ukuaji wa elimu hapa nchini.

Akipokea msaada huo Mkuu wa shule ye Sekondari ya Jitegemee Kanali Robert Kessy ameshukuru NIC kwa msaada huo ambao utasaidia kupunguza tatizo la uchakavu wa mabweni ya wavulana katika shule hiyo

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wameishukuru NIC kwa msaada huo na kuahidi kuyatunza mabweni yatakayo karabatiwa na kuyatumia kuongeza kiwango cha ufaulu.

Kwa mujibu wa Kanali Kessy Msaada huo wa NIC utasaidia kupunguza tatizo la uchakavu wa mabweni ya wanafunzi katika shule hiyo.