Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemsimamisha Mbunge wa jimbo la Ukonga mkoani Dar es Salaam, Jerry Silaa kuhudhuria mikutano miwili ya Bunge, baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya bunge hilo.
Akisoma bungeni taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mwenyekiti wa kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka amesema kamati imependekeza Silaa pia avuliwe uwakilishi wa Bunge la Afrika (PAP).
Wiki iliyopita Silaa aliitwa mbele ya Kamati hiyo akidaiwa kutoa kauli nje ya bunge kuwa Wabunge hawalipi kodi katika mishahara yao, jambo lililoelezwa kuwa ni uongo.
Mwakasaka ameliambia Bunge kuwa Silaa ni mkaidi na mjeuri, na kwamba ni mtu anayetakiwa kuangaliwa mienendo yake nje ya Bunge