Zaidi ya wanafunzi 2000 wenye ‘zero’ Mock kuanza kambi

0
143

Wanafunzi 2,098 (wakiwemo wanafunzi 50 wenye vipaji maalum) waliopata daraja sifuri katika mtihani wa Mock mkoa wa Simiyu wanatarajia kuanza kambi Septemba Mosi mwaka huu ili kujiandaa na mtihani wa Taifa.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Ernest Hinju ameyasema hayo wakati akipokea chakula kilichotolewa na wanachama wa klabu ya Yanga ikiwa ni kuunga mkono kambi ya kitaaluma ambapo amewashukuru na kusema mpango mkakati wa mkoa ni kuondoa sifuri na wanafunzi wenye vipaji wafaulu kwa daraja la kwanza na kuufanya mkoa kushika nafasi nzuri kitaifa.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Simiyu, Paul Susu ameshukuru kwa msaada wa chakula na karatasi za maandalizi ya mtihani huku mmoja wa wanafunzi wa kidato cha nne, Rita Masunga akiahidi kwa niaba ya wanafunzi wa Simiyu Sekondari kufanya vizuri mtihani wa kitaifa.

Kwa upande mwingine, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Dkt. Judith Ringia amewashukuru wanachama wa Yanga kwa kuchangia damu ili kuweza kuokoa maisha ya wagonjwa ambapo amesema uhitaji wa damu hasa kwa watoto na wajawazito.

Wakiwa Simiyu Sekondari wamekabidhi mchele kilo 100, unga kilo 50, maharage kilo 25, sabuni ya maji lita 15 na vifaa vya usafi.