Vifaa mbalimbali vyateketezwa

0
162

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza wameteketeza vifaa zaidi ya 70 vinavyotumika katika michezo ya kubahatisha, baada ya kubaini vimewekwa katika maeneo yasiyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria.

Vifaa hivyo vimeteketezwa baada ya Bodi hiyo kufanya operesheni maalum ya kupita katika mitaa mbalimbali ya jiji la Mwanza, operesheni iliyokuwa na lengo la kubaini Wafanyabiashara wanaokiuka taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.

Vifaa vingine vilivyoteketezwa ni vile vya bandia vilivyokuwa vikitumiwa na baadhi ya Wafanyabiashara ambao si waaminifu.