Timu ya watu wenye ulemavu yakaribishwa nchini Japan

0
1327

Timu ya watu wenye ulemavu kutoka Tanzania ikikaribishwa Tokyo nchini Japan inapofanyika michezo ya Olimpiki ya Walemavu (Tokyo 2020 Paralympic Games).

Kiongozi wa timu hiyo ni Tuma Dandi ambaye ni mtumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kocha ni Bahati Mgunda.

Washiriki kutoka Tanzania ni pamoja na Ignas Madumla anayeshiriki kurusha kisahani na Sauda Njopeka anayeshiriki kurusha tufe.

Michezo hiyo hiyo itakayohitimishwa tarehe 5 mwezi Septemba mwaka huu inashirikisha washiriki kutoka nchi 163.