Miili ya watumishi wa TRA yaagwa

0
273

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homerra ameongoza Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Mbeya pamoja na wakazi wa  jiji  Mbeya, kuaga miili ya Watumishi watano wa TRA mkoani humo waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Akizungumza wakati wa shughuli ya kuaga miili hiyo, Homerra amesema Taifa limepoteza vijana wachapakazi na wazalendo, ambao wamefariki dunia wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema vifo vya Watumishi hao vimeacha pengo kubwa kwa Taifa.
 
Watumishi hao watano wa TRA, walifariki dunia hapo jana baada ya gari aina ya Landcluser walilokuwa wakitumia kugonga kwa nyuma Lori aina Fuso.

Ajali hiyo ilitokea katika barabara ya Mbeya Tunduma eneo la Hanseketwa wilaya ya Mbozi.

Watumishi hao walikuwa kazini, ambapo inadaiwa walikuwa wakitumia gari hiyo kufukuza gari nyingine iliyohisiwa kubeba bidhaa za magendo.