Rais Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Zambia, kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Taifa hilo Hakainde Hichilema.
Sherehe za kuapishwa kwa Rais huyo Mteule wa 7 wa Zambia zinafanyika katika uwanja wa Taifa wa Mashujaa jijini Lusaka.
Marais wengine wanaoshiriki katika sherehe hizo ni pamoja na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Mokgweetsi Masisi wa Botswana na Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe