Serikali yapokea viti mwendo 100

Geita Tanzania

0
207

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amesema mafanikio yanayopatikana nchini katika kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo yanatokana na ushirikiano mzuri uliyopo baina ya serikali ya taasisi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.

Waziri Gwajima amesema hayo wakati akipokea viti mwendo 100 zenye thamani ya zaidi shilingi milioni 30 kutoka taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Plan International kwa ajili ya watoto wenye walemavu ili kuwawezesha watoto hao kuhudhuria masomo kwa watoto wa wilaya ya Geita.

Watoto hao wametolewa katika Kata za Kalangalala, Katoro, Kasamwa na Ihanamilo.

Waziri Dkt. Gwajima amepokea viti hivyo katika eneo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo.