Wakazi wa Pugu wafurahia mradi mkubwa wa maji

0
198

Wakazi wa Pugu na Gongo la Mboto wameipongeza serikali kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maji nchini ukiwemo mradi wa maji Pungu Gongo la Mboto uliokamilika wa asilimia mia moja.

Wakazi hao wamesema mradi huo ni mkombozi kwao kwani kwa sasa wameacha kutumia gharama kubwa ya kununua maji ya viwandani hali iliyokuwa ikiwarudisha nyuma katika shughuli za kiuchumi.

Wamesema hivi sasa baada ya mradi wa maji Pungu Gongo la Mboto kukamilika kwa asilimia mia moja wamekuwa wakitumia maji Safi na Salama yenye gharama nafuu hatua iliyochochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.

Aidha wakazi hao wamesema ni vyema sasa kwa Watanzania kuanza kuamini maji yanayotolewa kwenye miradi ya Serikali kwani ni mazuri na ni ya gharama nafuu ukilinganisha na bei ya maji ya Viwandani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesema Maji hayo ni Safi na salama kwani yanapitia katika mchakato wote wa hali kuwa Salama na wataalam wa kutibu maji.

Baada ya mradi huo kukamilika mapema mwaka huu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi amezuru kwenye mradi huo na kuridhishwa na uendelezaji wake huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya Maji na Mazingira yote ya miundombinu ya miradi ya maji ili iweze kudumu kwa muda mrefu.