Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuhudhuria mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kati ya Agosti 17 na 18 mwaka huu nchini Malawi.
Rais Samia anaondoka leo Agosti 16 akitokea jijini Dodoma. Kati ya mambo yatakayofanyika katika mkutano huo ni pamoja na kuithiboitisha Malawi kuwa mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja 2021/2022.
Matangazo ya mkutano huo yataruka mbashara kupitia TBC1, TBC TAIFA na TBCOnline.