Meli kubwa ya MV Yasemin mapema leo Agosti 14, imewasili katika Bandari ya Mtwara ikitokea nchi za Uarabuni ikiwa imebeba viuatilifu tani 2,850 kwa ajili ya kutibu magonjwa ya korosho.
Meneja wa Bandari nya Mtwara, Mhandisi Juma Kijavara amesema ujio wa meli hiyo ni matunda ya mikakati ya serikali na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha bandari hiyo inafanya kazi muda wote mara baada ya kukamilika kwa maboresho makubwa ambayo yalifanywa na serikali.
Akipokea meli hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ametaka viuatilifu hivyo viwafikie walengwa kwa wakati na wale wanaouza waache mara moja.