CEO wa Kampuni za Asas afariki dunia

0
160

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni za Asas (Asas Group of Campanies) Alhaj Faraj Ahmed Abri amefariki dunia alfajiri leo Ijumaa Agosti 13, 2021 mkoani Dar es Salaam.

Mazishi ya Asas ambaye ndiye mwanzilishi wa kampuni hizo yatafanyika leo baada ya Swala ya adhuhuri katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam.

Mzee Asas ni baba mzazi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Salim Abri.