Gharama ya kupima UVIKO-19 yapungua kwa asilimia 50

COVID-19

0
174

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepunguza gharama za upimaji wa Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19) kutoka dola za Marekani 100 hadi dola 50 kwa kipimo cha RT PCR.

Aidha, serikali imeondoa gharama za kipimo cha Antigen Rapit Test kwa maeneo ya mipakani, isipokuwa kwenye viwanja vya ndege ambapo wasafiri watalipia dola za Marekani 10 tu.

Serikali imeshusha gharama hizo baada ya kutenga kiasi fedha kulipia gharama za uendeshaji kwenye bajeti mwaka wa fedha 2021/2022

Hatua hii imefikiwa kufuatia ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Kenya Mei 4, 2021 na kutoa maelekezo ya kutatuliwa changamoto ya vibali na upimaji wa UVIKO-19 kwa abiria wanaovuka kupitia mipaka ya nchi kavu.