Watano wateuliwa

Ikulu Dar es Salaam

0
244

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi watano kushika nafasi mbalimbali serikalini leo Agosti 6, 2021 Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Samia amemteua Athumani Mbuttuka kushika nafasi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kufuatia kustaafu kwa Balozi wa Tanzania – Qatar, Mohamed Mtonga aliyekuwa akishika wadhifa huo.

Mgonya Benedict ateuliwa kuwa Msajili wa Hazina akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Mbuttuka.

Aidha, Rais amewateua Leonard Mkude, Frank Nyabundege na Casmir Kyuki kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uwekezaji ya UTT-AMIS, mtawalia.