Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiambatana na mkewe Mama Mbonimpawe Mpango amefika nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa, Kibaha Picha ya Ndege kutoa pole na kuifariji familia kufuatia kifo cha waziri huyo.
Makamu wa Rais ameweka saini katika kitabu cha maombolezo na baadaye kuzungumza na mke wa marehemu, Mareceline Kwandikwa ambapo amempa pole na kumuomba kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
Baadaye akizungumza na waombolezaji waliojitokeza nyumbani hapo, Dkt. Mpango amemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa na sifa za kipekee.
Amesema marehemu alikua mcha Mungu, mpole, mtulivu na mtu aliefanya kazi kwa uwezo wake wote. Amewataka waombolezaji kuendelea kuwa na moyo wa subira na kuiombea faraja familia ya Kwandikwa.