Makalla : Barakoa lazima

0
234

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ameagiza kuanzia sasa ni lazima kila mtu anayepanda kwenye chombo cha usafiri avae barakoa, na kwa vyombo vya usafiri (daladala) kupakia abiria kutokana na idadi ya viti.

Akizungumza na Waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam, Makalla amesema hatua hiyo ina lengo la kuzuia maambukuzi ya virusi vya corona.
 
Makalla ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kusimamia utekelzaji wa maagizo hayo, na kuhakikisha abiria yoyote asiye na barakoa hapandi kwenye chombo cha usafiri.
 
Kwa upande wa taasisi pamoja na ofisi zilizopo mkoani Dar es Salaam, ameagiza kuwepo na sehemu za kutakasa mikono na watu wote wavae barakoa.