Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mary Masanja akicheza ngoma ya asili ya Kimakonde katika eneo la mji mkongwe wa kihistoria uliopo Mikindani mkoani Mtwara.
Naibu Waziri huyo yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi, ziara yenye lengo la kukagua vivutio vya utalii vilivyopo mkoani humo ili viweze kuboreshwa na kutangazwa.