Tiketi kuona DABI zaanza kuuzwa

0
180

Wapenzi wa soka , leo wameanza kujitokeza katika mitaa malimbali ya Manispaa ya Kigoma, Ujiji kununua tiketi kwa ajili ya kushuhudia fainali ya kombe la Shirikisho kati ya timu za Simba na Yanga.

TBCOnline imeshuhudia
misururu mirefu ya mashabiki hao wa soka wakisubiri kununua tiketi ili waweze kushuhudia mtanange huo wa Simba na Yanga katika dimba la Lake Tanganyika.

Joto la mpambano huo wa watani wa jadi maarufu kama Debi ya watoto wa Kariakoo jijini Dar es Salaam limezidi kupanda mara baada ya kutangazwa bei za tiketi kwa ajili ya kuona mpambano huo pamoja na maeneo ya kuuzia tiketi hizo.

Redio ya TBC Taifa na TBCOnline itakuletea mbashara matangazo hayo na mengine mengi yanayojiri kutoka mkoani Kigoma, hasa kuhusu masuala ya soka na maendeleo ya miradi mbalimbali.