Zao la tangawizi kupewa kipaumbele

0
312

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Serikali itaendelea kulipa kipaumbele zao la tangawizi na kulipa heshima inayostahili.

Naibu Waziri Bashe ameyasema hayo wilayani Same mkoani Kilimanjaro, alipotembelea mashamba ya tangawizi katika kata ya Mamba Myamba, na kujionea changamoto mbalimbali zinazowakabili Wakulima wa zao hilo

Mara baada ya kujionea changamoto hizo, Naibu Waziri Bashe ameiagiza Tume ya Umwagiliaji mkoa wa Kilimanjaro kutembelea mifereji yote inayotumiwa na wakulima katika kulima zao la Tangawizi, na kufanya tathmini ya gharama zinazohitajika ili wizara iifanyie ukarabati.

Kwa sasa mkulima wa zao la tangawizi anavuna tani 10 katika hekta moja badala tani 30, kutokana na uchakavu wa miundombinu ya umwagiliaji uliyopo sasa katika kata hiyo ya Mamba Myamba,

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Malecela amesema ni wakati sasa wa wizara ya Kilimo kutatua changamoto zilizopo katika zao hilo, kwani Wakulima wamekuwa wakiteseka na kutumia gharama kubwa bila mafanikio.