Ujenzi wa hospitali ya kanda washika kasi

0
187

Muonekano wa jengo la hospitali ya rufaa ya Kanda ya Kusini inayojengwa mkoani Mtwara kwa ajili ya kuhudumia Wananchi wa mikoa ya Lindi, Ruvuma, Mtwara na nchi jirani ya Msumbiji.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo, ambao umekamilika Kwa asilimia 97.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ambaye anaanza ziara ya kikazi mkoani Mtwara hapo kesho, anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo tarehe 27 mwezi huu.