Ziara ya Dkt. Mpango yamfikisha kijijini kwake Kasumo

0
214

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, leo amewatembelea na kuwasalimu Wakazi wa kijiji cha Kasumo kilichopo wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, mahali alipozaliwa.

Akiwa kijijini hapo, Makamu wa Rais amewahakikishia Wakazi wa eneo hilo kuwa Serikali itatekeleza mambo yote yaliyopo katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 iliyoahidi katika wilaya ya Buhigwe na mkoa wa Kigoma kwa ujumla.

Amewashukuru Wakazi wa kijiji hicho kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Buhigwe hapo awali, na baadae kuendelea kushirikiana nae alipoteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amewasisitiza Wakazi wa kijiji cha Kasumo kuweka mkazo katika suala la elimu, na kuhakikisha wale wote wanaostahili kusoma wanapata haki hiyo.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango anaendelea na ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Kigoma.