Fifa yaipongeza klabu ya Simba

0
318

Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino ameipongeza klabu ya Simba kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2020/2021.

Katika barua yake kwa Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, Rais Infantino amesema ubingwa ni matokeo ya juhudi na kutekeleza majukumu kwa kila mmoja ndani ya klabu hiyo.

“Naomba uwasilishe pongezi zangu kwa kila mtu aliyehusika katika mafanikio ya Simba SC, na kuwatia moyo ushirikiano, ari na ushupavu,” amesema Rais Infantino Katika barua yake.

Pia amemkshukuru Rais Karia na TFF kwa kuchangia maendeleo na ustawi wa mpira wa miguu katika ukanda huu na duniani kwa ujumla.