Uongozi wa hospitali ya Mawenzi wavunjwa

0
195

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel ameuvunja uongozi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi kwa madai ya kushindwa kutatua kero za wagonjwa.

Naibu Waziri Mollel amefikia uamuzi huo wakati wa ziara yake hospitalini hapo na kuongeza kuwa, amekuwa akipokea malalamiko mengi kutoka kwa wagonjwa juu ya utendaji duni wa hospitali hiyo.

Kufuatia hatua hiyo, Naibu Waziri Mollel ameiagiza Idara ya Tiba na ile ya Rasilimali watu kutoka wizarani kuhakikisha inateua menejimenti mpya ya hospitali hiyo kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Seif Shekalaghe amesema amepokea maelekezo hayo ya Naibu Waziri na kuwataka Watumishi kufuata maadili ya kazi zao kila wanapotekeleza majukumu yao.