Mkuu wa mkoa wa Tanga, Adam Malima ameielekeza Idara ya Ardhi mkoani humo, kufanya sensa ya mifugo ili kutambua mkoa huo unaweza kuhimili mifugo kiasi gani.
Malima ametoa maelekezo hayo katika kikao kazi cha Watumishi wa Idara ya ardhi mkoa wa Tanga.
Amesema sensa hiyo ya mifugo itatoa mwongozo katika kupanga maeneo kwa ajili ya matumizi mifugo na makazi ya watu.
“Sisi Watanzania kiuhalisia zamani hatukuwa na asili ya kuthamini ardhi kama kipindi hiki, lakini pia mkoa wa Tanga una mambo mengi ikiwemo migogoro ya mashamba, ardhi na mipaka kwa sababu ya asili yake, hivyo sensa hiyo ni muhimu.” amesema Malima.