Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo kufuatia hasara kubwa waliyoipata kutokana na kuungua moto kwa siko hilo.
Kufuatia hasara kubwa iliyotokana na moto huo, Rais Samia ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina kujua chanzo cha moto huo.
Amesema Soko Kuu la Kariakoo ni soko kubwa jijini Dar es Salaam ambalo lina mkusanyiko mkubwa wa wafanyabiashara na kuteketea kwa moto kutakuwa kumesababisha hasara kubwa kwa wapangaji na wamiliki wa soko hilo kongwe nchini.
Rais amesema licha ya kuajiri wafanyabiashara wengi, Soko la Kariakoo ni kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki hivyo tukio hilo si hasara kwa wafanyabiashara tu bali hata kwa Serikali.