Wasioshiriki vikao, kukosa sifa za kugombea uongozi CCM

0
193

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewataka wanachama wa chama hicho kushiriki vikao kuanzia ngazi ya shina ili kutatua changamoto za wananchi.

Chongolo amesema mtu yeyote mwenye nia ya kuwa kiongozi anapswa kushiriki vikao ngazi ya shina ambapo kushiriki vikao hivyo itakuwa moja ya vigezo vitakavyofuatiliwa kwa wagombea katika ngazi yoyote.

Aidha Chongolo ameonya baadhi ya tabia ya wana-CCM kutengeneza makundi ya wagombea kuelekea uchaguzi wa viongozi wa chama mwakani, huku akisisitiza kuacha tabia ya kufuatiliana maisha ya mtu binafsi kwa kuchafuana kisiasa

Pia Katibu Mkuu huyo ametembelea baadhi ya miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwepo mradi wa shule ya wasichana mkoa wa Songwe, ambapo ameahidi kuchangia mifuko 200 ya saruji katika ujenzi wa shule hiyo ambao unaoendelea.

Chongolo yupo nyanda za juu kusini akiendelea na ziara ya kikazi, ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya shina.