Wachezaji wa Polisi Tanzania wajeruhiwa ajalini

0
315

Wachezaji kadhaa wa timu ya mpira wa miguu ya Polisi Tanzania wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani mkoani Kilimanjaro.

Chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa ni basi walilokuwa wakisafiria wachezaji hao kuacha njia na kugonga mti.

Habari zaidi kutoka mkoani Kilimanjaro zinaeleza kuwa, majeruhi wa ajali hiyo wanapatiwa matibabu katika hospitali ya KCMC mjini Moshi, huku baadhi yao hali zao zikielezwa kuwa ni mbaya.