Kituo cha madini John Magufuli kunufaisha wachimbaji

0
228

Mbunge wa Simanjiro mkoani Manyara Christopher Ole Sendeka, amesema kuzinduliwa kwa kituo cha ukusanyaji na uuzaji madini cha John Magufuli ndani ya mgodi wa madini ya Tanzanite cha Mirerani kitakua ni msaada mkubwa kwa wachimbaji wadogo katika eneo hilo.

Ole Sendeka amesema kuwa kumekuwa na udanganyifu katika uuzaji na uongezajj thamani wa madini hayo hivyo kuikosesha serikali mapato.

Akizungumza na TBC wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha madini cha John Magufuli, mbunge huyo amesema kuwa kituo hicho ni muhimu kwa sekta ya madini na kuitaka serikali kuongeza udhibiti wa usafirishaji wa madini ya Tanzanite.

Ameongeza kuwa kwa sasa bado kumekuwa na udanganyifu kwa wasafirishaji wa madini ya Tanzanite nje ya eneo la Mirerani na hivyo kuikosesha nchi mapato.