TBC ni sauti ya Watanzania

0
222

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Brigedia Jenerali Juma Sipe ameitaka TBC kuendelea kuwa sauti ya Watanzania kwa kutengeneza vipindi na kuripoti habari ambazo hazifungamani na upande wowote bali kuweka usawa kwa manufaa ya Tanzania.

Sipe ameipongeza TBC kwa utunzaji wa kumbukumbu za Redio Tanzania Dar es salaam (RTD), ambazo kwa sasa ni TBC Taifa.

Ametoa pongezi hizo mkoani Dar es Salaam, alipotembelea banda la Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) baada ya kuona vifaa vya zamani vilivyokuwa vikitumiwa na RTD pamoja na nyimbo za zamani za wasanii wa Tanzania.