Takribani milioni 540 kupeleka maji Mpanda

0
169

Serikali imeanza kutekeleza mradi mkubwa wa maji safi na salama wa Magula utakaohudumia wakazi zaidi ya 7,900 katika vijiji vya Matandalani Mtisi na Ibindi wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini- RUWASA wilaya ya Mpanda, Simon Kajange amesema serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 540 ili kukamilisha mradi huo.

Kajange amesema mradi huo umeanza kutekelezwa tangu Machi 18 na unatarajia kukamilika Julai 18 mwaka huu.

Pamoja na mradi huo kuhudumia wananchi wa vijiji hivyo, lakini pia wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu nao watanufaika na mradi huo.