Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya imetoa pikipiki kwa watendaji wake ili kuboresha utoaji huduma kwa wateja walioko pembezoni na kudhibiti upotevu wa maji.
Akikabidhi pikipiki hizo Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo, Edina Mwaigomole amewataka watendaji hao kuzingati mwongozo na taratibu za mamlaka hiyo ili kuzitunza pikipiki na kuzitumia kwa malengo yaliokusudiwa.
Awali mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Gilbert Kayange amesema kutolewa kwa pikipiki hizo kutaleta tija ya kuboresha huduma hasa maeneo yaliokuwa hayafikiwi kutokana na changamoto za usafiri.
Zaidi ya milioni 54 zimetumika kununua pikipiki hizo ambapo mbali na kuboresha huduma za maji, zitasaidia kukusanya maduhuli ya serikali.