Watanzania wahimizwa kutembelea vivutio vya utalii

0
167

Bodi ya Utalii kanda ya Ziwa imewahamasisha watanzania kuwa wazalendo na kujitokeza kutembelea vivutio vya utalii.

Akizungumza jijini Mwanza katika maandalizi ya Jukwaa la Vivutio vya Utalii,Eva Malya ambaye ni mkuu wa hifadhi kisiwa cha saa nane amesema ni jukumu lao kutunza na kuhifadhi rasilimali za utalii.

Pia amesema ni wajibu wao kuelimisha jamii kuhusiana na utalii,kutoa fursa za utalii ,fursa za uwekezaji na kutoa nafasi za Watalii kufurahia.