EOTF yawafunda Wajasiriamali

0
174

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na taasisi zinazojishughulisha na uwezeshaji Wananchi kiuchumi hasa makundi ya Wajasiriamali, ili kuinua sekta ya Wafanyabiashara wadogo.

Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda na Biashara Dotto James ametoa ahadi hiyo mkoani Dar es salaam wakati akifungua mafunzo ya Wajasiriamali wanaotarajiwa kushiriki maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam, mafunzo yanayosimamiwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).

Dotto amesema wizara ya Viwanda na Biashara inathamini jitihada zinafanywa na EOTF katika kuwainua na kuwawezesha Wajasiriamali kuboresha bidhaa zao na kuwa na mvuto sokoni.

Awali akizungumzia mafunzo hayo Mwenyekiti wa EOTFambaye pia ni mke wa Rais wa awamu ya tatu, Mama Anna Mkapa amesema wanatoa mafunzo hayo kwa lengo la kuwapa mbinu za kuyafikia masoko ya ndani na nje kwa wajasiriamali wa Tanzania.

Huu ni mwaka wa 24 kwa EOTF kutoa mafunzo na kusimamia ushiriki wa Wajasiriamali Katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam.

Mbali na Mama Mkapa wake wengine wa Viongozi wameshiriki mafunzo hayo ambao ni pamoja na Mama Marry Majaliwa, Mama Shadya Karume na Mama Regina Lowassa.