Poland kuisaidia Tanzania kuendeleza sekta ya mifugo

0
204

Tanzania imeishukuru Poland kwa mchango wake katika kukuza sekta ya mifugo nchini.

Shukrani hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa mambo ya nje wa Poland Pawel Jablonsiki ya kutembelea maabara mbili zilizoboreshwa kwa msaada wa nchi hizo zilizopo mkoani Arusha

Profesa Ole Gabriel ameiomba Poland kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha sekta za mifugo pamoja na uvuvi.

Kwa upande wake Naibu Waziri Jablonsiki amesema Poland imefurahishwa na ushirikiano uliopo baina yake na Tanzania kwa upande wa sekta ya mifugo ambapo imeahidi kuendeleza ushirikiano huo.

Ameeleza kuridhishwa na namna fedha ziilizotolewa na nchi hiyo zilivyotumika katika kuboresha maabara hizo.

Mbali na maabara hizo, wizara ya Mifugo na Uvuvi ina mpango wa kushirikiana Poland katika kuanzisha vituo vitatu vya umahiri ambapo kituo cha Tengeru kitakuwa kikihusika na masuala ya maziwa, kituo cha Mabuki masuala ya nyama na kituo cha Morogoro kitahusika na masuala ya ngozi.