Bajeti kuu 2021/2022 yapita

0
219

Bunge limepitisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 yenye jumla ya shilingi trilioni 36.3,  ikiwa ni ongezeko la asilimia 4 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2020/2021 iliyokuwa na shilingi trilioni 34.8.

Bajeti hiyo imepita baada ya Wabunge 361 ambao ni sawa na asilimia 94 ya Wabunge 385 kupiga kura za ndio.

Kura hizo zilikuwa za wazi ambapo kila Mbunge aliitwa jina lake na kusema ndio ama hapana.