Brg. Ndagala atunukiwa hati ya shukrani

0
213

Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma kimemtunuku hati ya shukrani aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Brigedia Jenerali Hosea Ndagala kwa mchango wake katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya kumkabidhi hati hiyo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kakonko Samoja Sadock amesema Brigedia Ndagala imekuwa kiongozi aliyefanya kazi yake kwa uzalendo na kutekeleza kwa vitendo shughuli mbalimbali za maendeleo kama ilivyoelekezwa kwenye ilani .

Naye katibu wa CCM wilaya ya Kakonko Abdul Kambuga amesema chama hicho wilayani humo kinajivunia kufanya kazi na kiongozi huyo kwani alikuwa msikivu na mwenyekujali na kusimamia maslahi ya wanakakonko.

Aidha chama hicho kimempongeza Brigedia Ndagala kwa kupandishwa cheo cha Kijeshi kutoka Kanali hadi Brigedia.