Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo mkoani Dar es salaam imemhukumu mshitakiwa Habinder Sethi aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kifungo cha nje na imemuamuru kulipa shilingi Bilioni 26 ndani ya kipindi cha miezi 12.
Mshtakiwa huyo amefanikiwa kulipa shilingi milioni 200 kati ya fedha hizo anazotakiwa kulipa ndani ya kipindi cha mwaka huo mmoja