Rais: CCM rekebisheni viwanja

0
193

Rais Samia Suluhu Hassan, amekitaka Chama Cha Mapinduzi kurekebisha viwanja vinavyomilikiwa na chama hicho na endapo watashindwa watafute mwekezaji.


Rais Samia amezungumza hayo jijini Mwanza laipokuwa akizungumza na vijana kitaifa wakiwakilishwa na vijana wa mkoa huo amabpo amesema CCM itumie fursa ya kuondolewa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyoondolewa kwenye nyasi bandia.


Pia ameiagiza Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo yakarabatiwe ili vijana watumie michezo kama fursa ya ajira.