Vijana watakiwa kutengeneza fursa za kijasiriamali

0
828

Wajasiriamali vijana nchini, wametakiwa kuwa na uchaguzi sahihi wa kufanya jambo ili kuwawezesha kufanya ujasiriamali kwa tija na mafanikio.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa ‘Maendeleo Bank’ Dkt. Ibrahim Mwangalaba wakati wa Kongamano la vijana la ujasiriamali, uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi yaliyoandaliwa na umoja wa vijana wa KKKT Jimbo la Kati Dayosisi ya mashaki na Pwani.

“Vijana wengi wemekuwa hawana uchaguzi maalum wa kutaka kujua Nini cha kufanya, nawasihi vijana lazima uwe na wazo ambalo unataka kufanyia Kazi ndipo uende kukopa pesa benki ili ufanye jambo lenye tija na unalolimudu,”- amesema Dkt. Mwangalaba

Kwa upande wake Mkuu wa Jimbo la Kati Mchungaji Frank Kimambo, amesema vijana wengi wanahitaji mafunzo kama haya ikiwa sambamba na mafunzo ya kiroho ili kuwa na tija ya mafanikio kiroho na kiuchumi.

Aidha Baadhi ya Vijana walioshiriki Kongamano hilo Anania Ndondole na Grace Adam, wamesema wamejifunza mengi juu ya uwekezaji na namna ya kufanya ujasiriamali wenye mafanikio na kilichobaki ni kwenda kutekeleza waliyojifunza kwenye kongamano hilo.