Makondakta waisafisha Mwanza kumkaribisha Rais

0
412

Na Sara Mollel

Umoja wa makondakta na wapigadebe mkoani Mwanza wamefanya usafi katika viunga vya mji huo ikiwa ni ishara ya kumkaribisha Rais Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuwasili mkoani humo Juni 13, 2021 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Makondakta hao wamezunguka sehemu mbalimbali kufanya usafi ikiwepo stendi ya mabasi Igombe, dampo na sehemu nyingine.

Mwenyekiti wa makondakta, Mlimi Juma amesema ni dhamira yao kuhakikisha mkoa wa Mwanza unakuwa safi na salama kipindi atakapokuwepo Rais na baada ya hapo.