Anayedaiwa kuua mama na watoto anaswa na polisi

0
230

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linamshikilia Shadrack Kapanga anayedaiwa kufanya mauaji ya watu watatu wa familia moja ambao ni mama na watoto wake wawili katika maeneo ya Masaki wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne  amesema kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa eneo la Magomeni akiwa katika harakati za kutoroka.

Amesema Shadrack Kapanga amekamatwa akiwa na baadhi ya vitu alivyoviiba ndani ya nyumba iliyokuwa ikiishi familia hiyo baada ya kufanya tukio hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda Muliro, upelelezi wa tukio hilo unaendelea ili kufahamu sababu za mauaji hayo na pindi utakapokamilika muhusika ama wahusika watafikishwa mahakamani.