Shule yapigwa tafu ujenzi wa madarasa

0
125

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jiji la Mbeya (Mbeya WSSA) imekabidhi bando 16 za bati zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sita kwa shule ya msingi Lwala iliyopo Mbeya vijijini, kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa vinavyojengwa kwa nguvu za Wananchi.

Akikabidhi bati hizo Afisa uhusiano wa mamlaka hiyo Neema Santos amesema kuwa, wametoa msaada huo baada ya kuona uchakavu wa baadhi ya majengo ya shule hiyo ya msingi Lwala, na hivyo kuzitaka taasisi nyingine nazo kuchangia ujenzi huo.