Dakik Balozi wa Mlima Kilimanjaro

0
151

Wizara ya Maliasili na Utalii imemteua Rawan Dakik kuwa Balozi wa Hiari wa Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kutambua jitihada zake za kutangaza Mlima Kilimanjaro, baada ya kupanda mlima huo mara tano na pia kuipeperusha bendera ya Tanzania katika kilele cha mlima mrefu zaidi duniani Everest uliopo bara la Asia.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (Mb) ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Rawan Dakik yaliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro leo.