Italia na Uturuki uso kwa uso UEFA EURO 2020

0
220

Mashindano ya mpira wa miguu ya kuwania kombe la Mataifa ya Ulaya (UEFA EURO  2020) yanaanza hii leo kwa kuzikutanisha timu za kundi A ambazo ni za mataifa ya Italia na Uturuki, mchezo utakaochezwa mjini Rome.

Mashindano hayo ya kuwania kombe la Mataifa ya Ulaya yanaanza hii leo baada ya kuahirishwa mwezi Machi mwaka 2020 kutokana na  ugonjwa wa corona.

Timu ya Taifa ya Italia ambayo haikufanikiwa kushiriki katika mashindano ya mwaka 2018, ina matumaini makubwa ya kushinda mechi ya leo kutokana na kushinda mechi zote 27 za hapo awali.

Hata hivyo, wachambuzi wa soka kutoka sehemu mbalimbali duniani wametaja uimara wa kikosi cha Taifa cha Uturuki, na kusema kuwa si cha kubezwa.

Mashindano hayo yatakayofikia tamati Julai 11 mwaka huu, yanafanyika katika miji 11 iliyopo katika mataifa mbalimbali.