Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limeongeza orodha ya majina ya vijana waliohitimu kidato cha sita wanaopaswa kujiunga na mafunzo kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2021.
Akizungumza jijini Dodoma kwa Niaba ya Mkuu wa JKT, Brigedia Jenerali Rajab Mabele, Kaimu Mkuu wa Utawala JKT, Kanali Hassan Mabena amesema vijana walioongezwa kuhudhuria mafunzo hayo wataungana na walioitwa hapo awali.
Aidha, Mabena amesema wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho wanapaswa kuripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani kutokana na kambi hiyo kuwa na miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu.
Katika mafunzo hayo vijana watajifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa lao.